Siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Kleruu CMF Sehemu ya Iringa wameendelea kuwa na mazoezi makali wakijifua kwaajili ya maandalizi ya mpambano mkali utakaohusisha Makanisa ya T.A.G yaliyopo Sehemu ya Iringa.
Mazoezi hayo ni maandalizi ya kuadhimisha kilele cha Wiki ya CMF Kitaifa, kwa Sehemu ya Iringa yatahitimishwa katika Viwanja vya Kleruu siku ya Jumapili 4/5/2014 kuanzia saa Tisa kamili Alasiri.
Zifuatazo ni picha za matukio ya J'mosi;
Wadau waliofika mapema mzoezini wakipeana dondoo mbili tatu
Baada ya kupeana dondoo na kufungua kwa maombi, mazoezi yakaanza;
Watumishi wa Bwana walikuwepo kushuhudia mazoezi
Kutoka kushoto ni Mch. Mlumbe, Mch. Kipemba, Mr. Bahati Msigwa na Bwn. Kaleb.
Mchungaji Kitine na Vijana wake naye pia alikuwepo uwanjani.
Baada ya Mazoezi, Wachezaji walijongea pembeni kupata nasaha kutoka kwa Wadau mbalimbali:
Mwisho wa Siku, Wachezaji wakakabidhiwa Jezi zao
Zoezi la kugawa Jezi lilisimamiwa na Mr. Emmanuel Chanai kutoka ICC
Baada ya kupewa jezi, wachezaji walitupia viwalo vyao
Picha ya juu Bwana Zakaria na Bwn Mbise wakiwa wamevalia jezi zao, picha ya chini wachezaji mbalimbali wakiwa ndani ya Jezi zao
No comments:
Post a Comment