Friday, 9 May 2014

TAMASHA KUBWA LA MICHEZO MAKANISA YA T.A.G SEHEMU YA IRINGA

Makanisa ya T.A.G Sehemu ya Iringa kupitia Idara ya Ushirika wa Wanaume wa Kikristo wameandika Historia mpya katika maadhimisho ya Kilele cha Sikukuu yao.

Katika kuadhimisha Kilele cha Sikukuu hii, CMF Sehemu ya Iringa waliandaa Tamasha kubwa la Michezo lililohusisha Makanisa yote ya T.A.G. Tamasha hili lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Kleruu; Michezo iliyokuwepo ni Mpira wa Miguu, Kuvuta Kamba, Kukimbiza Kuku na Kutembea na Yai likiwa kwenye Kijiko mdomoni; It was very funny kiukweli!!

Pamoja na Michezo hiyo, pia kulikuwa na Mahubiri ya Nguvu, Muhubiri alikuwa ni Mchungaji Mlumbe, Mwangalizi wa Sehemu ya Iringa.

Zifuatazo ni picha za Matukio hayo:

Katika Mchezo wa Mpira wa Miguu, ziliundwa Timu mbili;

Timu ya Kwanza ilihusisha Makanisa ya Ukanda wa Kihesa ambayo ni Kihesa, ICC (Sabasaba), Mtwivila, Mkimbizi, Ngome, Nduli, Kigonzile na Makanisa mengineyo yaliyopo ukanda huo. Timu hii ilivalia Jezi ya Bluu na nyeupe.

Timu ya Pili ilihusisha Makanisa ya Ukanda wa Mlandege ambayo ni Mlandege, Cornerstone, Mkwawa, Mawelewele, Zizi, na Makanisa mengineyo yaliyopo ukanda huo. Timu hii ilivalia Jezi ya Nyekundu.

Askofu wa Jimbo la Iringa Askofu Mkane pamoja na Jopo la Wachungaji wa Sehemu ya Iringa walikuwepo katika Tamasha hili.

Kandanda ilikuwa ya ukweli hadi kipindi cha kwanza kinaisha magoli ni moja kwa moja. Wakati wa mapumziko michezo mingine ikaendalea kama vile kuvuta kamba na kufukuza kuku.

Kuvuta kamba ilihusisha Makundi mawili; Kundi la Kwanza ni ICC walivutana na Mkimbizi na Kundi la Pili ni Mlandege walivutana na Kihesa. Kisha washindi wa kila kundi wakavutana na kumpata mshindi mmoja.

Kipute kilianza baina ya ICC na Mkimbizi; ngwe ya kwanza kamba ilikatika ikabidi kuunganisha kamba nyingi zaidi. Ngwe ya pili baada ya kamba kuunganishwa ICC na Mkimbizi wakaanza kuvutana tena, awamu hii ICC walikuja na Nguvu za hatari, waliwaburuza Mkimbizi hadi huruma aiseee!
Baadhi ya Wadau wa Mkimbizi ilibidi kuachia Kamba baada ya kuona wanaburutwa kwa spidi ya hatari, Mtumishi wa Bwana akaona isiwe kesi akaachia kamba;

Walifuatia Mlandege na Kihesa, ambapo Mlandege walifanikiwa kuwavuta Kihesa.
Mwisho wakakutana wababe ICC na Mlandege; Siku zote washindapo wawili lazima mshindi apatikane, Kwa taaabu sana Mlandege wakafanikiwa kuwa washindi.

Baada ya kuvuta kamba, ukafuata mchezo wa kufukuza kuku. Mchezo huu ulihusisha watu wazima wenye umri zaidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutoka Makanisa yote;

Baada ya Michezo hiyo, likafunguliwa Gombo la Chuo, Mchungaji Mlumbe akakabidhiwa kipaza sauti akatwanga Injili.

Wadau mbali mbali walijitokeza kwa wingi katika Tamasha hili;

Baada ya Mahubiri, Kipindi cha pili kiliendelea hadi kipenga cha mwisho Timu zilitoshana nguvu kwa magoli mawili kwa mawili. Wakaingia kwenye matuta, sintofahamu ikatokea baada ya Refarii kuwapa ushindi Mlandege kabla hawajamaliza kupiga penati. Then washindi wakakabidhiwa Ngao za ushindi;

Mwisho kabisa, Mchungaji Raphael Kitine akashusha maombi mazito, watu wakatawanyika kwa amani!

No comments:

Post a Comment