Ukifika kwa Mchungaji Raphael Kitine utakutana na geti moja la ukweli.
Mandhari ya nyumba ya Mchungaji wetu kwa kweli yanapendeza na kuvutiasana. Mchungaji Kitine ni mmoja wa Wachungaji mfano wa kuigwa na Wachungaji wengine kwa jinsi anavyotunza mazingira. Ukifika nyumbani kwake ki ukweli hutatamani kuondoka.
Baada ya kufika kwa Mchungaji Tulifanya Ibada ya Pamoja; Tuliongozwa na Neno toka Kitabu cha Waebrania 13:7; Unaozungumzia kuwakumbuka wanaotuongoza.
Baada ya Ibada, Mkurugenzi wa CA's ICC Mr. Ezekiel Fungo akazungumza dhumuni letu la kwenda pale, na kwaniaba ya Vijana akakabidhi zawadi kwa Mchungaji na Familia yake.
Baada ya kukabidhiwa zawadi Mchungaji alituombea Baraka Vijana wake na kutupa nasaha zake;
Mama Mchungaji Roswita Kitine naye alitupa nasaha zake, na kututia moyo tuendelee kumtumikia Bwana;
Kilichofuata ni kiburudisho cha nafsi kilichoandaliwa na Familia ya Mvchungaji Raphael Kitine;
Mwisho kabisa, tukapiga za pamoja kwa ukumbusho;
Viongozi wa CA's ICC; Kutoka kushoto ni Muhasibu wa Idara Bi. Rebecca Kawago, Mkurugenzi wa Idara Mr. Ezekiel Fungo na Makamu Mkurugenzi Bi. Joyce Senje wakiwa kwenye picha ya Pamoja na Mchungaji Raphael Kitine na Mama Mchungaji Roswita Kitine.
No comments:
Post a Comment