Sunday, 25 May 2014

UZINDUZI WA WIKI YA SIKUKUU YA IDARA YA WATOTO ICC

Mungu ni mwema wakati wote!

Hatimaye Idara ya Watoto ICC siku ya leo wamezindua rasmi wiki ya sikukuu yao ambayo itaanza kesho 26/05/2014 hadi Jumapili Ijayo 01/06/2014.

Ibada ya kwaza alihubiri mpakwa mafuta wa Bwana Mrs. O. Kipemba; Ujumbe ulikuwa ni muendelezo wa Somo la Kumtumainia Mungu, kwa siku ya leo alifundisha kuhusu "SABABU ZA KUMTUMAINIA MUNGU".

Akiwa amejaa upako zaidi ya maelezo, Mtumishi wa Bwana alielezea sababu kuu 3 za kumtumaini Mungu. Alifundisha somo hili kwa lugha ya Kiingereza akitafsiriwa na Miss. Joyce Senje.

 Alifundisha sababu kuu tatu, nitazitaja kwa ufupi somo kamili litawajia wakati mwingine.
1. Hatima ya maisha yetu ipo mikononi mwa Mungu.Yeremia 29:11, 1:5; Mathayo 6:25-33; Yohana 6:37
2. Mungu wetu ni msikivu, anasikiliza maombi yetu. Kutoka 3:7-8, Yermia 29:13
3. Mungu wetu huzitunza na kuzitimiza ahadi zake kwetu.  Hesabu 23:19;

Katika somo hili, alisisitiza kwamba;
> Mungu wetu kamwe hawezi kutufedhehesha,
> Mungu wetu kamwe hawezi kutuaibisha,
> Mungu wetu kamwe hawezi kututelekeza.

Alifundisha mambo mengi hayo ni kwa ufupi tu, mwisho alihitimisha kwa maombi;

Ibada ya pili ndio ulifnyika uzinduzi rasmi, ambapo Watoto wote, Waalimu wa Watoto, pamoja na Wadhamini wa Idara ya Watoto waliingia kwa maandamano.


Baada ya kuingia ndani na kupitiliza hadi Madhabahuni, Mwalimu Mkuu wa Idara ya Watoto Mr. Nico William alsema jambo kuhusu siku hii na kuomba ushirikiano toka kwa Waamini wote ili kufanikisha sikukuu hii ya Idara ya Watoto.

Kilichofuata Ibada ya Kusifu na Kuabudu iliendelea kwa kushirikisha Timu ya Kusifu na Kuabudu ikiongozwa na Miss Joyce Senje, Watoto na Kanisa zima kwa ujumla.

Kifupi Ibada ya Kusifu na Kuabudu ilijaa uwepo wa Mungu, na kila aliye mruhusu Roho wa Bwana hakutoka patupu.



Mtumishi wa Bwana Mr. Joseph Fungo huwa ana nibariki sana hasa wakati wa kusifu na kuabudu, huyu Bwana aisee hata sijui nimuelezee vipi. Yaani huwa anasifu kama vile ndo kapewa nafasi ya mwisho kusifu baada ya hapo anatwaliwa. Ki ukweli inapendeza na inabariki sana, anajua nini anachokifanya.

Upande wa muziki alikuwepo Mwl. Nuhu kwenye Keybord na Bw. Barnaba Haran gitaa la base.

Kama kawaida, kila mtu na wito wake, kikazi zaidi!

Ibada ya pili alihubiri Mchungaji wa Idara ya Watoto, Mrs. Roswita Kitine ambaye ni Mama Mchungaji kiongozi wa ICC.


Alifundisha somo linalosema "MUNGU ANA MPANGO NA WATOTO WETU", alifundisha kwa ufupi tu kama utangulizi na uzinduzi wa Wiki ya Sikukuu ya Watoto. Alifundisha kuwa mpango wa Mungu kwa Watoto ni kuhubiri Injili pamoja na Wazazi wao wala si kuwaacha nyuma.
Maandiko: Yeremia 1:4-7; Marko 16:15-16; Mathayo 28:19-20; Yoel 2:28; Rumi 10:15

Kwa jinsi alivyofundisha somo hili kwa muda mfupi ila kwa upako wa hali ya juu sana, watu wengi waliguswa. Mwisho akatoa wito kwa watu ambao wapo tayari kutumika katika Idara ya Watoto waende mbele, watu wengi walijitokeza wakafanyiwa maombi maalum.

Kulikuwa na makundi ya aina tatu:
1. Watu ambao wapo tayari kumtumikia Mungu katika Idara ya Watoto kwa kujitolea kwenda kufundisha Neno la Mungu mashuleni;
2. Watu ambao wapo tayari kumtumikia Mungu katika Idara ya Watoto kwa njia ya kuwawezesha Waalimu watakaokwenda kufundisha Mashuleni;
3. Watu ambao wapo tayari kumtumikia Mungu katika Idara ya Watoto kwa kujitolea kuwa Wafadhili wa Idara kwa ujumla.

Makundi yote matatu yalifanyiwa maombi na Mchungaji Kiongozi Mch. Raphael Kitine, akishirikiana na Mchungaji wa Idara ya Watoto Mrs. Roswita Kitine.


Mwisho Mchungaji kiongozi alitoa Baraka zake na kuzindua rasmi sikukuu ya Watoto.

Baada ya hapo Ibada ikaahrishwa kwa maombi, tukatawanyika kuelekea majumbani.

Nje ya kanisa wadau wakabadilishana mawazo mawili matatu kabla ya kwenda nyumbani.

Mungu ametubariki ICC katika nyanja zote; wenye magari wapo, wenye bodaboda wapo, wenye baiskeli wapo na wasugua soli pia tupo. Muhubiri 3:1


Siku ndo ikawa imekamilika kiivo yaani!
Ubarikiwe, karibu sana ICC, mualike ndugu, jamaa na rafiki yako.

No comments:

Post a Comment