Sunday, 18 May 2014

LEO IBADANI ICC: HATUA MUHIMU ZA KUPOKEA MUUJIZA WAKO

Ibada ya leo ICC ilikuwa nzuri sana yenye Uwepo wa Mungu kiasi cha kutosha. Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine kafundisha somo zuri sana lilimgusa kila mtu kuhusu "Hatua Muhimu za Kupokea Muujiza Wako". Kabla ya Neno kulikuwa na Ibada ya kusifu na kuabudu kama ilivyo ada!

Leo timu ya kusifu na kuabudu iliongozwa na Mr. Andrew Magelanga pamoja na Miss. Joyce Senje.


 Upande wa Muziki, Keyboard alisimama Kijana Daniel Makombe, Gitaa la besi lilikamatwa na Mwl. Nuhu



Upande wa dawati la IT alikuwepo kijana mtanashati Mr. Nico William kuhakikisha matangazo, nyimbo  zinapaa hewani vizuri, pia set up mbalimbali za kidigitali;

Kwaya Iliyohudumu ni kwaya ya PATMO


Ibada ya kusifu na kuabudu ilikuwa nzuri sana yenye uwepo wa Mungu, kwa yeyote aliyefungua moyo wake alipokea kitu;






Baada ya kusifu na kuabudu kilifuatia kipindi cha Mahubiri, katika Ibada zote mbili alihubiri Mch. Raphael Kitine, ujumbe ulisema "Hatua Muhimu za Kupokea Muujiza wako"
 Mchungaji Raphael Kitine (Kulia) akihubiri Ibada ya kwanza ya Kiingereza, sambamba naye ni Mtafsiri wake Mr. Edom Fungo (Kushoto). Miaka kadhaa ijayo nikisikia Edom kawa Pastor wala sitashangaa hata kidogo, dalili za mvua ni mawingu.

Ibada ilikuwa na Nguvu sana, Mchungaji alihubiri kwa Uweza na Nguvu za Roho Mtakatifu isivyo kawaida.


Baada ya Mahubiri (Ujumbe kamili utaupata hapahapa) kuhusu hatua muhimu za kupokea muujiza wako, alitoa nafasi kwa watu mbalimbali kushuhudia  matendo makuu au muujiza ambao Mungu amefanya.

Mtu wa kwanza kutoa ushuhuda alikuwa ni Mtafsiri wake Mr. Edom Fungo, ambaye alishuhudia uponyaji wa Mungu kwani wiki nzima amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya jino hasa nyakati za asubuhi, hadi anapanda madhabahuni kutafsiri hali haikuwa shwari. Baada tu ya kukanyaga madhabahu ya Bwana akapokea uponyaji, Utukufu kwa Bwana.


Baada ya Bwana Edom kufungua pazia la kushuhudia, Waumini kadhaa nao walipata nafasi ya kumshuhudia Mungu japo kwa ufupi kutokana na muda kuwa hautoshi.





Ibada ya pili nayo ilikuwa moto wa kuotea mbali


Katika Ibada ya Leo kulikuwa na matukio kadhaa, ikiwemo Mchungaji Raphael Kitine na Familia yake kununua Speaker kubwa moja aina ya Fidek na kuikabidhi kwa Viongozi wa Kanisa kwa niaba ya Kanisa zima. Mungu akuzidishie Baba.





Tukio jingine, Mr. & Mrs Edom Fungo walimshukuru Mungu kwa kuwabariki mtoto wa kike waliyempa jina la Alice.


Shukrani hazikuishia hapo, Binti Glory Chanai  (aliyeshika Microphone) naye pia alimshukuru Mungu kwa kumponya kwenye ajali ya pikipiki a.k.a bodaboda.


Somo kamili la leo "HATUA MUHIMU ZA KUPOKEA MUUJIZA WAKO"litawajia hapahapa, usitoke usiondoke. Pia ntembelea ukurasa wetu wa facebook, iringacentralchurch.
UBARIKIWE.

No comments:

Post a Comment