Tuesday, 6 May 2014

MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKUKUU YA CMF - I.C.C YAFANA SANA

Siku ya Jumapili ya Tarehe 4/5/2014 Wanaume wa Makanisa yote ya T.A.G walihitimisha Wiki ya Sikukuu yao.
Wanaume wa Kanisa la Mahali pamoja la Iringa Central Church (ICC) Sabasaba nao waliadhimisha Sikukuu hiyo kwa namna ya kipekee sana iliyompendeza kila mtu aliyehudhuria Kanisani.

Mchungaji Raphael Kitine akinena jambo katika Sikukuu hiyo

Mwenyekiti wa CMF ICC akiwatambulisha watenda kazi wenzake wa CMF - ICC
Kutoka kushoto ni Mr. Emmanuel Damalo (Mwenyekiti), Mr. Respicius Kahabuka (Makamu Mwenyekiti), Mr. Gerald Malekela (Katibu), Mr. Emmanuel Chanai (Mtunza Fedha) na Mr. Edom Fungo (Mtunza Fedha Msaidizi)

Baada ya kutambulisha watenda kazi, Mwenyekiti aliwaita Wanaume wote wapite mbele ya Kanisa.

Baada ya Wanaume kupita mbele wakaimba wimbo kwa pamoja

Baada ya Wanaume kuimba, ilifuatia Comedy moja ya hatari, watu walicheka sana lakini pia ujumbe ulifika kupitia Comedy hiyo. Comedy ilifunguliwa na Mr. Damalo & Gerald;

Comedy iliendelea, Mr. Edom & Barnaba wakachukua nafasi; Aisee, it was very funny!! Never seen Before.

Kanisa lote kwa ujumla ilikuwa ni full burudani;

Mchungaji Kiongozi wa I.C.C Mch. Raphael Kitine naye alishindwa kujizuia kucheka, akaachia tabasamu la nguvu la Kikuhani..

Ibada ya Kusifu na Kuabudu ilifuatia, Wanaume walijijimimina mbele za Bwana zaidi ya maelezo.

Kwa upande wa Muziki mambo yalikuwa mazuri, Kijana Daniel Makombe aliitendea haki keyboard, kwa nyuma Mwl. Nuhu akiwa sambamba na gitaa la bass.

Baada ya Kipindi cha Kusifu na Kuabudu, kilifuatia kipindi cha maombi na maombezi yaliyosimamiwa na Mchungaji Kiongozi Raphael Kitine akishirikiana na Mch. O. Kipemba.

Kisha Mahubiri yakafuatia ambapo Mpakwa Mafuta wa Bwana na ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi wa siku hiyo Mchungaji Mwanafunzi Omega Kipemba, akiwa amejaa upako isivyo kawaida alihubiri somo "MWANAUME NA UAMSHO". Ki ukweli huyu Mtumishi wa Bwana ni Jembe la Yesu, linakwatua hata kwenye udongo mgumu; sina zaidi la kuongeza ila Waamini wa ICC Sabasaba wanamfahaamu vyema.

Waamini wa ICC walifuatilia Mahubiri kwa umakini mkubwa sana.

Siku hiyo Watu walikuwa ni wengi sana Kanisani, ikabidi baadhi ya Wanaume watoe mabenchi nje ya Kanisa na kukaa huko huku wakifuatilia michakato yote inayoendelea..

Baada ya Mahubiri, Wanaume wa ICC wakamtia moyo Mlezi wao Mch. Raphael Kitine kwa kumpa zawadi kidogo. Mpango mzima ulisimamiwa na Mwenyekiti wa CMF ICC kwa kushirikiana na Wanume wote pamoja na Mgeni Rasmi MCh. O. Kipemba.

Mchungaji Kiongozi, akazungumza jambo kuwashukuru Wanaume, na kuwatia moyo waendelee kuifanya kazi ya Bwana kwa bidii.

CMF I.C.C ikawekwa Wakfu rasmi kwa Viongozi wake kufanyiwa Maombi mazito na Mch. Raphael Kitine, kisha wakapiga picha ya pamoja;

Mwisho kabisa kuna Familia mbili zilitoa sadaka ya shukrani.
Familia ya kwanza ni Mr. & Mrs. Mkocha walimshukuru Mungu kwa kupata Mtoto wa Kiume ambaye ndiye First Born kwenye Familia yao, Mungu awatie Nguvu mumlee Mtoto wenu katika njia ya Haki.
Pia Mrs. Mgavilenzi naye alimshukuru Mungu kwa mambo mengi ambayo Bwana amemfanyia.

Ibada iliahirishwa kwa Maombi, Waamini wote wakakaribishwa kwenye Tamasha kubwa la Michezo katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Klerruu ili kuihitimisha Wiki ya Sikukuu ya Wanaume (CMF).
Nje ya Kanisa baadhi ya Wanaume wakapiga picha mbili tatu;

Dondoo chache za Uwanjani:

Askofu Mkane na Jopo lake walikuwepo Uwanjani:

Mpira wa Miguu ulikuwa kati ya Ukanda wa Kihesa na Ukanda wa Mlandege. Ukanda wa Kihesa ulihusisha makanisa ya Kihesa, ICC Sabasaba, Mtwivila, Mkimbizi, Ngome n.k; Ukanda wa Mlandege ulihusisha Makanisa ya Mlandege, Cornerstone, Mkwawa, Mawelewele n.k
Kikosi Cha 1: Ukanda wa Kihesa

Kikosi Cha 2: Ukanda wa Mlandege

Refa alikuwa Mr. Mlandali kutoka Chuo cha Ualimu Klerruu akisaidiwa na Mr. Timiza Lwisa toka Mlandege na Mr. Zelaiko Nyamoga toka ICC Sabasaba.

Burudani nyingine ilikuwa kuvuta kamba, ICC tulianza kuwaburuza Mkimbizi vibaya sana, tukaingia fainali na Mlandege..

Matukio zaidi ya Tamasha la Michezo, yatawajia hapahapa; usitoke usiondoke. Stay tuned.




6 comments:

  1. I like that! may the Lord God Bless ICC and its Pastor R. Kitine without forgetting all members of ICC. Naona Bwana anafufua kazi ya mikono yake.

    ReplyDelete
  2. safi sana icc ni kweli, na mnafanya vizuri sana, big up msimamizi wa blog hii.

    ReplyDelete
  3. naamini hili litakuwa jambo kubwa sana katika dunia ya sasa hasa kizazi hiki cha .com.
    pia ni vema ratiba za ibada ziwe wazi tu muda wote kwenye blog kama picha, sio hadi kuseach ili mtu yeyote akiingia tu aone moja kwa moja., coz wengine wavivu kutafuta tafuta ndani ya blog, ila mengineyo blog ipo poa inaedelea kushine tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli Mtumishi wengine Kutafuta ndani ya blog ni tatizo; Ukiangalia vizuri upande wa kulia chini ya picha ya Mchungaji kuna ratiba ipo hapo, so huitaji kutafuta ndani. Japo ndani ukitafuta utaipata pia. Ubarikiwe.

      Delete