Thursday, 1 May 2014

Ziara ya CMF I.C.C Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa

Katika kuadhimisha Wiki ya Sikukuu ya Ushirika wa Wanaume wa Kikristo (CMF), Wanaume wa Iringa Central Church (ICC), Kanisa linaloongozwa na Mch. Raphael Kitine, siku ya leo wamefanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa.

Zifuatazo ni picha zinazoonesha ziara hiyo jinsi ilivyokuwa.

Ukifika tu Hospitali ya Rufaa Iringa utakutana na Bango hili

Baada ya Wanaume wa ICC kufika, walichukua picha ya pamoja.
Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa CMF ICC Mr. Emmanuel Damalo, akifuatiwa na Mr. Joseph Fungo, Mr. Beto Nguyu, Mr. Respicius Kahabuka (Makamu Mwenyekiti), Mr. Raphael Chiza, Mr. Daniel Juma Pharey, na mwisho ni Mr. Ezekiel Fungo.

Baada ya kuwasili, wakakutana na Bango linaloonesha mpangilio wa Wodi za Wagonjwa.

Ziara ikaanza, ikiongozwa na Mr. Damalo na Mr. Kahabuka, kwa nyuma Mr. Fungo J. akihakikisha usalaama wa Wanaume:

Ziara ikiendelea

Kabla ya kuingia Wodini wakapeana mikakati nini cha kufanya watakapoingia Wodini;

Baada ya kupeana mikakati wakaanza kuingia wodi moja baada ya nyingine

Watumishi wa Bwana hawakwenda mikono mitupu, walibeba vijizawadi vidogo vidogo kwa ajili ya kuwapatia Wagonjwa; kama vile sabuni, mafuta n.k; "Eee bana Mikono mitupu hailambwi"

Hawakuishia kugawa zawadi ndogondogo tu, bali walitimizo Agizo kuu la Bwana Yesu, enendeni Ulimwenguni kote mkahubiri injili, pia mtu hataishi kwa mkate tuu..
Wanaume walihubiri Neno la Mungu na kufanya Maombezi kwa Wagonjwa wakiongozwa na Jembe la Yesu Bwn. Ezekiel Fungo.

Watumishi wa Bwana hawakuishia hapo, walikwenda hadi Wodi TATA, Wodi ambazo kutembelewa ni nadra sana, Wodi amabayo hata ukianza kukemea yakupasa ukemee ukiwa hujafunga macho, mlango wa Wodi ukiwa wazi, ikiwezekana uwe umezaa Helmet na umefanya mazoezi ya riadha kidogo, otherwise anything can happen!!
Kwenda kutembelea Wodi hii , inabidi Roho wa Bwana awe amesema na Wewe kwelikweli, vinginevyo utashindwa kujua uliingilia mlango gani, uliingia pekua au ulikuwa na viatu, ulikuwa na shati umechomekea na tai au ulikuwa na singlend tu a.k.a kawosh!! Wodi hii nadhani ulishaitambua, inaitwa Wodi ya Vichaa. Kichaa ni kichaa tu.

Nimefanikiwa kupata picha mbili tu za Watumishi wa Bwana wakitoka ndani ya Wodi hiyo; Itabidi Bwn. Gerald Enock Malekela atueleza kinagaubaga kilichotokea ndani ya Wodi hiyo:
Ni jambo la kumshukuru Mungu, Watumishi wa Bwana wametoka Wodi ya Vichaa salama salimini bila ya kuwa na manundu.

Credits to Mr. Gerald Malekela kwa kufanikisha zoezi zima la uchukuaji wa matukio ya leo, Mungu akubariki sana Kaka.Stay tuned.

2 comments:

  1. To God all be the Glory this Church Has made Great Life changes To Many People, Be Christian it is an actions which Bless the people. I Warmly welcome Other people to visit this Blog to Learn Many things which will Transform their Lives. Glory Be To God ICC. You have made an Impacts to Others people lives.Especially by visiting people in Iringa Hospital and pray with them. I am Much Blessed.

    ReplyDelete