Friday, 2 May 2014

Mazoezi ya CMF Sehemu ya Iringa

Wanaume!! Taifa Kubwa...
CMF!! Ee Bwana Fufua Kazi yako..

Jumapili ya Tarehe 4/05/2014 itakuwa ni kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Sikukuu ya Ushirika wa Wanaume wa Kikristo (Christian Men's Fellowship - CMF). Katika kuadhimisha kilele cha Wiki hii ya Sikukuu, Wanaume wa Sehemu ya Iringa watakutana kwa pamoja katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Klerruu ambapo watafanya bonanza la Michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbia kwa kupokezana vijiti, kukimbia kwa magunia n.k pamoja na Mkutano wa Injili.

Ili kufanikisha mpango huo, Wanaume wa Sehemu ya Iringa hukutana Viwanja vya Klerruu kwaajili ya kufanya mazoezi. Siku ya Leo kutakuwa na mazoezi kabambe kuanzia saa tisa kamili jioni. Tafadhali wewe mkazi wa Iringa usikose.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za mazoezi yaliyofanyika siku ya Mei mosi katika viwanja hivyo.
Wanaume wakijifua uwanjani

Kweli Wanaume wamedhamiria, hata walipoambiwa kuvua mashati ili kumrahisishia Refa kazi ya kuwatambua wachezaji wa Timu pinzani, kwao haikuwa tatizo, Wanaume na heshima zao walivua mashati-vitambi nje kandanda likapigwa..

Nje ya Uwanja kama kawaida, wapendwa walikuwepo kuwapa sapoti wenzao;

Baada ya mazoezi, Wanaume wakakusanyika kupeana mawili matatu..

Mjasiri haachi asili, mtangazaji maarufu wa kituo cha redio cha Nuru FM Mkoani Iringa Ndg. Gerald Malekela naye alikuwepo katika mazoezi, baada ya mechi kazi na dawa, hakuondoka patupu;
Ndg. Gerald Malekela akifanya mahojiano na Ndg Emmanuel Damalo ambaye ni Mwenyekiti wa CMF kanisa la ICC.

Video clip fupi wakati wa Mazoezi yakiendelea;

No comments:

Post a Comment